Machapisho

MUNGU YU UPANDE WAKO SIKU ZOTE

      Katika maisha ya Mwanadamu kuna mengi tunayopitia na vikwazo tunavyokutana navyo,lakini bado lipo tumaini na uweza ulio mkuu toka kwa Mungu Bab a. Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.  Isaya 43:2 Maana mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako.  Isaya 43:3            @.. Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nwe --Mungu yuko pamoja nasi hata tupipo katika shida ngumu namna gani katika maisha tunayokutana nayo hapa duniani,tupitapo katika maji mengi,ni ile hali ya kuwa na taabu nyingi sana na mateso ambayo kwa akili zetu za kibinadamu hatuwezi ila mpaka Msaada wakr Mungu.                @.. Uendapo katika moto hautatekete --Haijalishi ni maumivu kiasi gani unapitia katika maisha hat...

IMANI ILIYO KUU ITENDAYO KAZI NDANI MWAMINI NDANI YA KRISTO YESU.

@..Imani ni kuwa na hakika na mambo yatalajiwayo na bayana ya mambo yasio onekana. 1..kwa imani tunaamini Mungu ndiye muumba wa mbigu na nchi. 2..kwa imani tunapokea uweza na nguvu kutoka kwa Mungu. 3..kwa imani tunapokea uponyaji na tumepewa mamlaka ya kuponya wasio jiweza.                 MATHAYO 9 VS 20 @Kwa imani mwanamke aliamini akigusa pindobla vazi la Yesu atapona.        Kuna mambo 3 aliyoazimia moyoni mwake mwanamke huyu. 1.. kwanza alikuwa na imani moyoni mwake wala hakuwa na shaka. 2.. Aliamini hata Yesu asipomuombea ila akigusa pindo la vazi lake atapona. 3.. aliamini Yesu anaweza kuponya ugonjwa wake. Nb.. katika yote unayoyapitia katika maisha yako ya ka siku katika maisha haya yatupasa kuwa na imani iliyo kuu ndani ya KRISTO YESU na pasipo kuwa na shaka lolote.. #Mwakalinga Imani @The_Day_Of_Glory @mwakalinga26@gmail.com

IMANI

Picha
πŸ”˜NENO LA UZIMA LEO. Somo.IMANI.Webrania 12. Shaloom Shaloom. πŸ”²Je, umewahi hisi bwana amekurudi/amekuadhibu? Wakati umemwani sana na  unampenda.? Nawasilimia mno, leo tuangalie kipengele hiki kwa kina *KURUDIWA NA MUNGU*  Na nina karibisha mawazo yako na uchangie leo.. *Webrania 12:5-14* πŸ–‹5 tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye; πŸ–‹6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. πŸ–‹7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? πŸ–‹8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. πŸ–‹9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? πŸ–‹10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali y...

IMANI ITENDAYO KAZI

✝ *NENO LA UZIMA LEO* ( *Prayer Worries Minisrry*) πŸ“–Somo. *IMANI.* Mpendwa Bwana Yesu Asifiwe Sana, tunaendelea kuangalia sura ya 11. Ya kitabu cha Waebrania. ✍🏽 *Leo naomba tupitie Waebrania 11:13-16.* 13 Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi. πŸ–Š14 Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. πŸ–Š15 Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea. πŸ–Š16 Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji. 🟀Maandiko haya nimuendelezo wa mistari iliyopita 7-12. Ikiwazungumzia Mababa wa Imani au watu wakwanza kutendembea na Mungu kwa Imani tangu wale wale wa gaharika mpaka wale waliotembea katika Agano la Mungu , kina Enoch, Abraham, Nuhu, Sarah, Nk. *Mambo Makuu 3 Yakujifunza kwao.* 1. *Walimwamini tu  Mungu hata  k...

Kusudi la Mungu kwa mwanadam

​BE PART OF CHANGE​ DHAMBI......ni uasi unaomuweka mwanadamu mbali na uso wa Mungu.....Mungu anapokuwa anamuita mwanadamu kwa sauti ya upole na mwanadamu anapopi nga sauti  ya Mungu,Mungu naye humuuacha mwanadamu afuate tamaa za moyo wake na uchafu wa kila namna,na mara nyingi mtu wa namna hii huishia njia ya upotevuni japo kusudi la Mungu ni kila mwanadam kuishi maisha ya Utakatifu na kumpendeza yeye ​ warumi..1:24​ ​ Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao,waufuate uchafu,hata wakavunjiana heshima ya miili yao​. Kumbuka tupo katika dunia iliyojaa kila aina ya uchafu na inawezekana bado hujajuwa ni uchafu wa namna gani hapa..tazama kuna mengi yanayofanya tuonekane wachafu na tusiofaa mbele za Mungu 1...dhambi za siri ambazo tunajuwa binadamu yoyote hakuoni ila juwa Mungu anatuona,uzinzi uasherati,masengenyo,chuki na mengine mengi ambayo hayafai mbele za Mungu.... Ndg.....bado mda upo wa kuanza upya na Mungu hujach...

Yesu ndiye mchungaji mwema

https://youtu.be/J4FRp3EeHr8

01..TAMBUA SABABU ZA WEWE KUWEPO DUNIANI

     ..Maisha ya mwanadamu huanza kwa kusudi maalumu,yawe ya kimwili au ya kiroho. Huwa kuna sababu kuu ambayo MUNGU ameweka ndani ya kila mwanadamu,lakini kama wanadamu tumeshindwa kujuwa na kutambuwa nini hasa kusudi LA Mimi kuwepo hapa dunian.      TAMBUWA UKUU WA MUNGU NDANI YA MAISHA YAKO...     KIla mwanadamu awaye yeyote chini ya juwa kuna kitu maalum ambacho Mungu ameweka ndani ya maisha ya kila mmoja, Kalama na vipawa mabalimbali vyote Mungu aliweka ndani ya mwanadam,lakini sasa wanadamu tumekuwa ni watu ambao tunashindwa kutumia kalama zetu na vipawa vyetu kama Mungu anavyotaka.              Habakuki ..2:1-      Mimi nitasimama katika zamu yangu,nitajiweka juu ya mnara,nitaangalia ili nione atakaloniambia,na jinsi nitakavyojibu juu ya kulala mika kwangu. Sasa kama wanadamu ambao tunajuwa kabisa kwamba tuna nia ya dhati kuwa ndani yangu n...