IMANI
Somo.IMANI.Webrania 12.
Shaloom Shaloom.
๐ฒJe, umewahi hisi bwana amekurudi/amekuadhibu? Wakati umemwani sana na unampenda.?
Nawasilimia mno, leo tuangalie kipengele hiki kwa kina *KURUDIWA NA MUNGU*
Na nina karibisha mawazo yako na uchangie leo..
*Webrania 12:5-14*
๐5 tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye;
๐6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.
๐7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?
๐8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.
๐9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?
๐10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
๐11 Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.
๐12 Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza,
๐13 mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.
๐14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
*Kwanini Mungu Anaturudi?*
๐1. Ni upendo wake kwetu, hufanya ivyo ili kuonesha upande mwingine wa yeye alivyo kama Mungu lakini pia kama Muumbaji wa mwanadamu (Ana utu wa ubinadamu). Mungu ni mwenye wivu sana juu ya mwanadamu hapendi aabudu au tu Amini kitu kingine zaidi yake. Kumbuka anguko la mwandamu Eden.
๐2. Ni kwa faida Yetu wenyewe, kwani ni heri kurudiwa na Mungu kuna usalama zaidi mikononi mwake.
๐kuturudisha kwake yeye, Mungu huachilia/ Huruhusu baadhi ya mambo magumu ili yakuvute zaidi kwake... Kumbuka Ayubu alikua mkamilifu katika mambo yote lakini bwna aliruhusu magumu..
Usiache imani yako kwasababu ya ugumu fulani fulani.
Barikiwa na Bwana.
⭕Leo karibuni tufanye mjadala juu ya mistari hiyo, Shuhuda zako zitatujenga..
Pst.latson
latsonmusa5@gmail.com
WordoflifeMission
Maoni
Chapisha Maoni