01..TAMBUA SABABU ZA WEWE KUWEPO DUNIANI
..Maisha ya mwanadamu huanza kwa kusudi maalumu,yawe ya kimwili au ya kiroho.
Huwa kuna sababu kuu ambayo MUNGU ameweka ndani ya kila mwanadamu,lakini kama wanadamu tumeshindwa kujuwa na kutambuwa nini hasa kusudi LA Mimi kuwepo hapa dunian.
TAMBUWA UKUU WA MUNGU NDANI YA MAISHA YAKO...
KIla mwanadamu awaye yeyote chini ya juwa kuna kitu maalum ambacho Mungu ameweka ndani ya maisha ya kila mmoja,
Kalama na vipawa mabalimbali vyote Mungu aliweka ndani ya mwanadam,lakini sasa wanadamu tumekuwa ni watu ambao tunashindwa kutumia kalama zetu na vipawa vyetu kama Mungu anavyotaka.
Habakuki ..2:1-
Mimi nitasimama katika zamu yangu,nitajiweka juu ya mnara,nitaangalia ili nione atakaloniambia,na jinsi nitakavyojibu juu ya kulala mika kwangu.
Sasa kama wanadamu ambao tunajuwa kabisa kwamba tuna nia ya dhati kuwa ndani yangu nina kitu ambacho Mungu ameweka ndani yangu,yanipasa kusimama na kuchukuwa hatua ya dhati kabisa katika kumuuliza Mungu ili aweze kunisaidia,maana inafikia kipindi tunakuwa ni watu wa kulalamika na sio watendaji wa kazi ya Mungu,habakuki alikuwa ni mtu wa kulalamika lakini badaye aliona kuna haja ya kusimama katika zamu yangu kama mtumishi wa Mungu ili aone ni kitu gani ambacho Mungu atamwambia,hivyo nawe ndugu yangu yatupasa kuchukuwa hatuwa madhubuti kabisa katika kumuliza Mungu,ili aweze kuinua kalama na vipawa vilivyomo ndani yetu,maana nina uhakika hivyo ulivyo kuna kitu ambacho Mungu ameweka ndani ya kila mmoja ili uweze kusaidia wengine nao wapate uheri.
Zaburi..73:16
Nami nilifikilia jinsi ya kufahamu hayo,ikawa taabu machoni pangu
Yawezekana unatafakali sana juu ya namna gani unaweza kuunza kutumia kipawa chako katika maisha,na unaona inakuwa ngumu sana kwako ila sasa kwa akili na ufahamu wetu kiukweli hatuwezi katika kutenda hayo,ila kwa msaada wa Mungu na ROHO MTAKATIFU twaweza kuyatenda yote,maana yeye ndiye msaada wetu na kimbilio letu katika maisha ya KIROHO,
Muhubili 9:1a...
Na kwa ajili ya hayo yote,nikatia moyo wangu katika kuyatafuta-tafuta haya
Kumbe yote twayaweza kwa kuwa tuna nia thabiti mioyoni mwetu juu ya kutenda kazi ya Mungu ipasavyo ila kama tutakuwa na mikono legevu hatutaweza kufikisha kweli ya Mungu katika kusema kweli yake.
Kumbuaka Mungu huwa atafuti watu kwa ajili ya kutenda kazi yake ila Mungu hutafuta mtu atakayesimama na kutete kweli yake yawezekana ni mimi au ni wewe,hivyo basi ni jukumu letu sote kuchukuwa hatuwa kwa moyo wa dhati na kuanza kazi ya Bwana Mungu....
MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUCHUKUWA MDA WAKO NA KUSOMA SOMO HILI.
@Evengelist imani mwakalinga..
Whasp 0629112471/0676560578
@mwakalinga26@gmail.com/imanmwaka@gmail.com
@facb..Imani mwakalinga
Twetter..Imani mwakalinga
Maoni
Chapisha Maoni