IMANI ITENDAYO KAZI

✝ *NENO LA UZIMA LEO*

  • ( *Prayer Worries Minisrry*)


📖Somo. *IMANI.*
Mpendwa Bwana Yesu Asifiwe Sana, tunaendelea kuangalia sura ya 11. Ya kitabu cha Waebrania.

✍🏽 *Leo naomba tupitie Waebrania 11:13-16.*
13 Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.
🖊14 Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe.
🖊15 Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea.
🖊16 Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.
🟤Maandiko haya nimuendelezo wa mistari iliyopita 7-12. Ikiwazungumzia Mababa wa Imani au watu wakwanza kutendembea na Mungu kwa Imani tangu wale wale wa gaharika mpaka wale waliotembea katika Agano la Mungu , kina Enoch, Abraham, Nuhu, Sarah, Nk.

*Mambo Makuu 3 Yakujifunza kwao.*

1. *Walimwamini tu  Mungu hata  kufa bila kuziona zile Ahadi.*
Tangu mwanzo 3:15. Ndipo pana historia ya Mungu kuanza kutembea na watu wake ili atengeneze kizazi au uzao utakaomponda kichwa joka..
Yaani mpango wa ukombozi..

Alianza kutembea na watu wake katika nyakati hizo na kuwapa maelekezo pamoja na Ahadi, wengi hawakuziona walikufa lakini hawakuicha imani yao.
🖋usimwache Mungu kwa sababu ya mambo fulani hayajatokea mapema ulivyo dhani. Mungu anampango mkubwa sana kuliko mawazo yako.

2. *Tumani lao halikua Hapa Duniani*
Hawakua na mpango wa kumiliki au kukaa duniani milele walijua kua wao ni wasafiri tu na wapitaji..
Kumbuka Abraham na Lutu ndunguyake palipo tokea ugomvi juu ya ardhi ya kulisha mifugo yao Abraham aliamua kumuachia Lutu ile Ardhi nzuri na yenye rutuba ya kutosha hakua na tamaa ya umiliki juu ya nchi.

3. *Walitarajia mji ulio bora Mbinguni*
✒Toka mbali huko walikua na tumaini la kwenda kumuona Mungu juu Mbinguni hivyo walikaza imani yao na kumtumaini Mungu tu bila kitu kingine.

✒Leo hii watu tunaishi hali tumepoteza uelekeo kabisa hatuna tafakari bora juu ya hatima yetu ya umilele, na wapi tunaenda baada ya maisha haya..

✒Nakushauri leo Imani uliyoipokea katika kristo Yesu ni ya umilele, kukupeleka katika Mji bora wa kristo Yesu juu mbinguni.
Dunia hii inapita na vyote. Kama ilivyo haribiwa na Mungu wakati wa gharika itapita tuu..

Ubarikiwe na Yesu.

  Ev.Imani Mwakalinga
mwakalinga26@gmail.Com
Prayer worries ministry

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KWANINI UFIE DHAMBINI WAKATI NEEMA IPO

🌳BADO TUMAINI LIPO USIKATE TAMAA🌳