KWANINI UFIE DHAMBINI WAKATI NEEMA IPO

Napenda kuchukuwa fulsa hii kumshukulu Mungu muumba wa Mbingu na Ardhi kwa uweza na nguvu zake,hata leo tuko hai ni kwa neema tuu na upendeleo wake. Pia napenda kukushukuru wewe mpenzi msomaji wa makala hii kwa kuchukuwa mda wako na kuweza kupata nafasi ya kusoma juu ya nini ROHO WA MUNGU anasema na watu wake kwa njia ya usomaji. Kwa maaana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtowa mwanawe wa pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele,UZIMA WA MILELE ni maisha anayoishi mtu akiwa hai hapa ulimwenguni pia na baada ya ufufuo wa milele.. Katika maisha tumekuwa ni watu ambao tunatenda mambo tofauti na mapenzi ya Mungu kitu ambacho kinatuletea madhara makubwa sana katika maisha yetu ya kiroho na kimwili,na hatimaye kupoteza Utukufu wa Mungu kabisa ndani yetu,ila sasa kusudi la Mungu ni kila mtu aishi maisha ya kumpendeza ye...