🌳BADO TUMAINI LIPO USIKATE TAMAA🌳
Daudi akasema nilikuwa kijana sasa ni mzee sijawahi ona mwenye haki wa MUNGU ameachwa,wala watoto wake kuomba omba mitaani.....
USIVUNJIKE MOYO.......
Ni kweli pindi tunapokutana na tatizo huwa tunaumia sana na hata kukata tamaa kabisa ya maisha na kuona kwamba huna msaada wala hakuna tena tumaini jipya,usikate tamaa lipo tumaini....
LIPO TUMAINI JIPYA.....
Kumbuka sasa kwamba MUNGU anasema nini juu ya mwanadamu na nini mpango wa MUNGU juu yako..
Yeremia 32:27
Tazama mimi ni MUNGU wa wote wenye mwili,je?kuna jambo lolote nisilo liweza.
Utaona kwamba yote tunayokutana nayo ni mapito tuu katika ulimwengu huu ,lakini pindi ambapo tunakutana na matatizo tunasahau kama yupomfaliji wa pekee mungu muumba aliye tufanya kwa mfano wake.
Tunapita katika mambo mengi...Magonjwa
...Misiba
...Na mambo mengine mengi kama hayo .
Yeye ni Mungu wa wote wenye mwili mpe shida na taabu zako zote yeye anaweza.
Yelemia 33:3
Mungu anasema niite anami takuitikia,takuonyesha mambo magumu usiyo yajuwa,.
Kumbe tukimuita Mungu ana kumueleza shida zetu yeye atasikia na kutujibu haja zetu,pia kutuonyesha hata yale tusioyajuwa katika maisha yetu...
MWAMINI MUNGU NA UMTEGEMEE YEYE PEKEE YAKE.
Iman Mwakalinga........
Maoni
Chapisha Maoni