KWANINI UFIE DHAMBINI WAKATI NEEMA IPO

            Napenda kuchukuwa fulsa hii kumshukulu Mungu muumba wa Mbingu na Ardhi kwa uweza  na nguvu zake,hata leo tuko hai ni kwa neema tuu na upendeleo wake.

Pia napenda kukushukuru wewe mpenzi msomaji wa makala hii kwa kuchukuwa mda wako na kuweza kupata nafasi ya kusoma juu ya nini ROHO WA MUNGU anasema na watu wake kwa njia ya usomaji.

            Kwa maaana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtowa mwanawe wa pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele,UZIMA WA MILELE ni maisha anayoishi mtu akiwa hai hapa ulimwenguni pia na baada ya ufufuo wa milele..

Katika maisha tumekuwa ni watu ambao tunatenda mambo tofauti na mapenzi ya Mungu kitu ambacho kinatuletea madhara makubwa sana katika maisha yetu ya kiroho na kimwili,na hatimaye kupoteza Utukufu wa Mungu kabisa ndani yetu,ila sasa kusudi la Mungu ni kila mtu aishi maisha ya kumpendeza yeye na hatimaye kuufikia uzima wa milele,na hata kuulithi ufalme wa Mbingu,na sio kuishi maisha ya dhambi ambayo yanatuweka mbali na Mungu.

             Kumbukumbu la Tolati 30:19
                      
                 NAZISHUDIA MBINGU NA ARDHI MBELE YAKO LEO,KUWA NIMEWEKA MBELE YAKO UZIMA NA MAUTI,BARAKA NA LAANA,CHAGUA UZIMA BASI ILI UISHI WEWE NA KIZAZI CHAKO.

Kuna mambo ambayo Mungu ameweka mbele yetu kama wanadamu tuna machaguo juu ya hayo,Uzima na Mauti lakini Mungu alivyo wa Rehema anasema mwanangu chaguwa Uzima basi ili uishi na si kingine.
         UZIMA NI NIN..??
                                Kumtii Bwana Mungu wako na kuisikia sauti yake na kushikamana naye,na huo ndio uzima wako wewe na kizazi chako,au kuenenda sawasawa na mpango wa Mungu na kufuata maagizo ya Neno lake kama anavyotaka yeye huo ndiyo mpango na kusudi la Mungu kwa mwanadamu,

         MAUTI NI NIN....??
                                 Ni kifo au hali ambayo mtu anakuwa amekata puuzi yake na hayupo tena dunia,pia mauti inaweza ikawa ya kimwili au kiroho mtu anaweza akawa amekufa roho yake lakini mwili bado tunaona ni mzima kabisa,JE MTU ANAKUFAJE ROHO YAKE? Kufa roho ya mtu ni pale mwanadamu anapotoka katika kusudi la Mungu na kufuata mambo yake binafsi ambayo ni tofauti kabisa na mpango wa Mungu,na kuendelea kufanya mambo ya dunia kama uzinzi,uasherati,fitna,ufisadi na mengine mengi kama hayo.
        Mfano.....Mtu alikuwa anamtumikia Mungu kwa nguvu zake na akili zake zote pindi anapoanza kwenda tofuti na kusudi la Mungu ndipo hapo dhambi huingia ndani ya mtu huyu na asipojilekebisha inaweza kuleta umauti katika maisha yake.

Kumbuka Neema ya Mungu bado ipo usikae katika dhambi ambayo itakuweka mbali na uso wa Mungu,jua na utambuwe Mungu wetu ni wa rehema na anaupendo nasi,ni jukumu lako sasa kuchukuwa hatuwa na kuanza kuishi maisha mapya ya Utakatifu,kumbuka Mungu huwa hapendi mwanadamu aliyemuumba kwa mkono wake na kwa mfano wake afe katika dhmabi.

          CHUKUWA HATUWA SAA YA WOKOVU NI SASA,USIPOTE AU KUFA KATIKA DHAMBI KWA AJILI YA STAREE ZA DUNIAN ZA MDA MFUPI,MTAFUTE BWANA MAADAMU ANAPATIKANA.

Evengelist.Imani Mwakalinga
imanmwaka@gmail.com
0629112471/0764477185/0676560578
imanimwakalinga@yahoo.com
                            

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

IMANI ITENDAYO KAZI

🌳BADO TUMAINI LIPO USIKATE TAMAA🌳