MUNGU ANAPIGANA UPANDE WAKO

Je ni nani unayemtegemea  katika pito lako,au katika magumu yako unayoyapitia katika maisha yako.

Je wajuwa kuwa yupo Mungu awezaye yote na yeye ni yote ndani ya yote ukiwa upande wake atakushindia,na ambaye hajawahi shindwa na gumu lolote,

           2 nyakati 32:7
                               🎄iweni hodari na wenye moyo mkuu,msiogope,wala msifadhaike kwa ajili ya mfalme wa Ashuru,wala kwa majeshi walio pamoja naye;maana yupo mkuu pamoja nasi kuliko aliye pamoja naye.

🎄Kumbe utaona sasa kumbe tatizo haliko kwa Mungu tatizo liko kwetu wanadamu tunakuwa watu ambao hatuna uhakika na Mungu aliye hai,kumbe yatupasa kuwa hodari kwa yale tunayopitia katika maisha yetu ya Kiroho na kimwili yawe na ushuhuda na kumpendeza Mungu,haijalishi watu wanakupiga vita kiasi gani au unapitia katika magumu kiasi gani,usife moyo mwite Mungu aliye hai,ambaye yeye ni yote ndani ya yote,.
                  NIKO ALIYEKO ATAKAYE KUWAKO NDIYE BWANA WA MAJESHI  ANAYETUSHINDIA NA ZAIDI YA KUSHINDA.


Mwakalinga imani
0629112471/0764477185
imanmwaka@gmail.com
imanimwakalinga@yahoo.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KWANINI UFIE DHAMBINI WAKATI NEEMA IPO

IMANI ITENDAYO KAZI

🌳BADO TUMAINI LIPO USIKATE TAMAA🌳