eps 1.đź“–BADO MUNGU NI WA HURUMA KWETUđź“–

Napenda kuchukuwa fulsa hii kumshukuru Mungu kwa Upendo wake wa ajabu katika maisha yetu,maana kama si yeye nani angesimama na kusimulia matendo yake makuu juu ya maisha yetu...

          ⛪Kiukweli wanadamu tumekuwa ni watu ambao tunajisahau sana,na imefika kipindi tunafanya mambo yetu kama vile hakuna Mungu,hata kusahau ni pendo la namna gani ambalo Mungu alionesha kwetu sisi kama wanadamu,je !? Ni upendo wa jinsi gani mtu kufa kwa ajili ya wengine...

                      Yohana mtakatifu 3:16
             ⏰Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtowa mwanae wa pekee,ili kila amwaminie asipote bali awe na uzima wa milele.

            ⛪Kumbuka Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu mimi na wewe ili tuweze kupona,alichukuwa uchafu wangu na mabaya yangu yote ya kila namna ili mimi niwe huru,lakini kama wanadamu tumekuwa ni watu ambao tumekuwa na mioyo migumu sana.Dhambi ndiyo ilifanya Mungu amtowe mwanae kwa ajili yetu lakini bado kama wanadamu tumekuwa niwatenda dhambi afadhali ya sodoma na gomola,dhambi za uzinzi sasa mpaka makanisani ni kitu cha kawaida kusemana vibaya ni kawaida ,huyu anachuki na yule na bado wote wanasema tunaenda mbinguni na sijiwi ni mbigu gani hiyo tunayoelekea,Kiukweli Mungu atusaidie katika hili,Ili hasira ya Mungu isije ikawaka juu yetu kama wakati wa Nuru.
          ⛪Ndugu yangu hebu tugeuke basi maana upendo wa Mungu kwetu ni mkuu sana kuliko jinsi tunavyowaza katika akili zetu kama wanadamu,maana yeye hutuwazia mema kila wakati katika maisha yetu......
          BADILIKA......

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KWANINI UFIE DHAMBINI WAKATI NEEMA IPO

IMANI ITENDAYO KAZI

🌳BADO TUMAINI LIPO USIKATE TAMAA🌳