🌹KUSUDI LA MUNGU KWA MWANADAMU
Mungu alimfanya mwanadamu kwa mfano wake na ndiyo maana akamtofautiaha na vyote vilivyomo duniani,
Na kusudi la Mungu ilikuwa ni kila mtu aishi maisha ya UTAKATIFU.
Lakini sasa binadamu wa leo tumegeuka na kuangalia mambo yetu zaid kuliko kuangalia Mungu anasema nini kuhusu Kanisa,na kila mtu kuishi akiwa na hofu ya Mungu ndani yake,
Utaona katika kitabu cha
Yakobo 4:1-
Anawauliza vita vyatoka wapi mapigano yaliyomo kati yenu yatoka wapi,si humu katka tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu.........
Utagunduwa kuwa hata leo makanisa huyu hamtaki huyu na huyu haongei na huyu na wote tunajiita watu tulio okoka na tumekombolewa na damu ya Yesu,ule upendo wa kweli haupo watu wanapenda vyeo na pesa makanisani kuliko kutafuta uso wa MUNGU,dhambi haisemwi tena makanisani kisa watu watapunguwa na sijuwi ni mbigu ya namna gani tunayoelekea.
Lakini bado MUNGU anatupenda na kuvumilia yote hayo
Yakobo 4:7-8
Basi mtiiini Mungu,mpingeni shetani naye atawakimbia,
Mkalibieni MUNGU naye atawakalibia
Kumbe yatupasa kugeuka na kuacha yote ya ulimwengu ,na kuachili yote tulionayo baina ya huyu na yule na kuutafuta uso wa MUNGU na haki yake naye atajifunua kwetu,na kufungua milango katika maisha yetu....
Imani mwakalinga.........
Maoni
Chapisha Maoni